Wednesday, May 6, 2020

ILI KAHAWA ISITAWI VIZURI INAHITAJI:

Ni muhimu kupanda kwa mistari na kwa nafasi; kutegemeana na aina ya kahawa na zao linalochanganywa.
Arabika:
futi (9x 9) = (mita 2.7 x 2.7)
Robusta:
Chotara: futi (9 x 4.5) = (mita 2.7 x 1.4)
NJIA ZA KUZALISHA MICHE YA KAHAWA
Kuna njia nyingi za uzalishaji wa miche ya kahawa ambazo nazo ni
• Mbegu
NB: Mbegu zinazotokana na mibuni ya chotara zisitumike kuandaa miche.
• Vichipukizi
• [Kupitia Maabara (Tissue culture)]
a. UZALISHAJI WA MICHE BORA
Miche bora huzalishwa kwenye vituo vya utafiti wa kahawa, au wakulima waliopata ujuzi toka kwenye vituo vya Utafiti wa kahawa kama vile: vikundi mbali mbali vya uzalishaji ambavyo vimethibitishwa na vituo hivyo.
b. JINSI YA KUZALISHA MICHE
Mbegu huoteshwa ardhini au kwenye viriba, miche iliyo oteshwa kwenye viriba huwa na nguvu zaidi, hivyo huhimili zaidi mazingira magumu shambani.
Sifa zinazofaa kwa kitalu
• Kitalu kiwe na kivuli na uzio kuzuia upepo mkali
• Udongo uwe na rutuba ya kutosha.
• Udongo usiotuamisha maji
• Kiwe karibu na maji ya kutosha
• Kiwe karibu na barabara
KUPANDA MBEGU
• Mbegu zipandwe mapema ili wakati wa kuhamishia shambani zikutane na msimu wa mvua.
• Nafasi kati ya mche na mche senti mita 15 x 15
• Miche hukaa kitaluni kwa muda wa miezi 10-12, wakati huo huwa na wastani wa sentimita (20-30).

No comments:

Post a Comment

KUVUNA

  Kahawa hua tayari kuvunwa miezi 8 hadi 9 kutoka kipindi ambacho maua ya mechomoza unatakiwa kuvuna matunda ambayo yam...