Wednesday, May 6, 2020

KUVUNA







 Kahawa hua tayari kuvunwa miezi 8 hadi 9 kutoka kipindi ambacho maua ya mechomoza unatakiwa kuvuna matunda ambayo yamesha yamesha iva na kubadilika rangi kua nyekundu .
— Ukivuna matunda ambayo bado hayaja iva usababisha kahawa kua chungu sana
— Katika maeneo ya kitlopikia unaweza kuvuna mara moja kwa mwaka.

MAANDALIZI YA SHAMBA


Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kuanzisha shamba la
kahawa ni pamoja na
• Mahali panapofaa kupanda kahawa
• Aina ya udongo
• Kiasi cha mvua
• Mwiinuko
• Joto
• Usafishaji wa shamba
• Upimaji wa nafasi ya kupanda
• Uchimbaji mashimo
• Uchanganyaji mbolea kabla ya kupanda.
Katika kuandaa shamba la kupanda kahawa miti mikubwa na miamba mikubwa hung’olewa
Kwa maeneo ambayo yanaweza kutifuliwa mbolea kama phosphorus inatakiwa kuwekwa mara nyingi shambani kabla ya kuamishia mche shambani. Na maeno ambayo hapawezi kutifuliwa mashimo huweza kuwekwa na buldoza.
Mashimo ni lazima yawe makubwa na yenye kina kirefu  kuwezesha kutovunja mizizi wakati wa kuhamishia mimea shambani.
Kahawa hupandwa kwa kutumia miche ambayo imekuzwa kwenye vifuko.
Nafasi ya kupada ni 3m x 3m kwa kiasi cha mimea 1280 kwa hekta (/ha).
— Miti ya kivuli kama vile Leucaena au migomba inaweza kupandwa kwa 6m x 6m.




ILI KAHAWA ISITAWI VIZURI INAHITAJI:

Ni muhimu kupanda kwa mistari na kwa nafasi; kutegemeana na aina ya kahawa na zao linalochanganywa.
Arabika:
futi (9x 9) = (mita 2.7 x 2.7)
Robusta:
Chotara: futi (9 x 4.5) = (mita 2.7 x 1.4)
NJIA ZA KUZALISHA MICHE YA KAHAWA
Kuna njia nyingi za uzalishaji wa miche ya kahawa ambazo nazo ni
• Mbegu
NB: Mbegu zinazotokana na mibuni ya chotara zisitumike kuandaa miche.
• Vichipukizi
• [Kupitia Maabara (Tissue culture)]
a. UZALISHAJI WA MICHE BORA
Miche bora huzalishwa kwenye vituo vya utafiti wa kahawa, au wakulima waliopata ujuzi toka kwenye vituo vya Utafiti wa kahawa kama vile: vikundi mbali mbali vya uzalishaji ambavyo vimethibitishwa na vituo hivyo.
b. JINSI YA KUZALISHA MICHE
Mbegu huoteshwa ardhini au kwenye viriba, miche iliyo oteshwa kwenye viriba huwa na nguvu zaidi, hivyo huhimili zaidi mazingira magumu shambani.
Sifa zinazofaa kwa kitalu
• Kitalu kiwe na kivuli na uzio kuzuia upepo mkali
• Udongo uwe na rutuba ya kutosha.
• Udongo usiotuamisha maji
• Kiwe karibu na maji ya kutosha
• Kiwe karibu na barabara
KUPANDA MBEGU
• Mbegu zipandwe mapema ili wakati wa kuhamishia shambani zikutane na msimu wa mvua.
• Nafasi kati ya mche na mche senti mita 15 x 15
• Miche hukaa kitaluni kwa muda wa miezi 10-12, wakati huo huwa na wastani wa sentimita (20-30).

Tuesday, May 5, 2020

FAHAMU KWA KINA KUHUSU KILIMO CHA KAHAWA

UTANGULIZI
Kahawa ni miongoni mwa mazao ya biashara ya biashara yanayoliingizia taifa mapato mengi, kahawa ni zao la pili la biashara baada Tumbaku.
Asili:kwa mujibu wa wataalam asili ya kahawa ni katikati ya Ethiopia.
kusambaa: kutoka Ethiopia kahawa ilisambaa hadi India, Uturuki, Italia, Uingereza na Africa mashariki
  1. Tanzania–Hulimwa sehemu tofauti tofauti ikiwemoMiteremko ya Mlima Kilimanjaro na kusini mwa Mlima Meru, Nyanda za juu za Ngorongoro, Miteremko ya Milima ya Uluguru, Kaskazini mwa Mkoa wa Mara (Hususani wilaya ya Tarime), Mkoa wa Kigoma (Wilaya za Kasulu, Kibondo), Mkoa wa Mbeya wilaya za Rungwe, Mbeya, Mbozi and Na Tanga katika miteremko ya Milima ya Usambara.
  2. Kenya– Hulimwa maeneo ya Ol Donyo Sabuk, Machakos, Nakuru na Rift Valley.
  3. Uganda– Hulimwa Maeneo ya Bugisu Mlima Elgon, Kigezi, Ankole, Toro na Nile

KUVUNA

  Kahawa hua tayari kuvunwa miezi 8 hadi 9 kutoka kipindi ambacho maua ya mechomoza unatakiwa kuvuna matunda ambayo yam...